Moran AI · Tanzania

AI agent anayejibu wateja wako WhatsApp saa 24

Weka namba yako ya WhatsApp Business, ongeza bidhaa na bei zako, na Moran anaanza kujibu wateja mara moja: bei, stock, picha, delivery, order na booking, kwa Kiswahili na Kiingereza. Ukihitajika, anakuita.

Anza bure siku 5 Ongea nasi

Kwa nini biashara za Tanzania zinatumia Moran

Wateja wanaandika "bei?", "ipo?", "mnaleta Mbezi?" saa nne usiku na wanataka jibu sasa. Moran anajibu mara moja kutoka kwenye data yako halisi, anahesabu jumla, anaweka order, na anakukumbusha wewe na mteja kabla ya delivery au appointment.

Anajibu mara moja, usiku na mchana

Bei, stock, maeneo ya delivery, saa za kazi, picha: majibu ya papo hapo kutoka kwenye data yako, si kubahatisha.

Anaongea kama wateja wako

Kiswahili, Kiingereza au mchanganyiko, hata ujumbe mfupi wa mtaani kama "bei?", "kmy", "upo?".

Anauza, si kujibu tu

Anahesabu bati 50 × bei, anaweka order, anapanga delivery au pickup kwenye calendar, na anafuatilia mteja mwenyewe.

Inafanyaje kazi

Unganisha namba yako

Namba yako ya WhatsApp Business inaunganishwa kupitia Meta Embedded Signup rasmi. Hakuna coding.

Weka bidhaa na maelezo ya biashara

Bidhaa, bei, stock, picha, gharama za delivery, sera. Agent anasema tu kilicho kwenye data yako.

Mwache afanye kazi

Anajibu wateja, anaweka order na booking, anahifadhi kila mteja na jina lake na anakotoka, na anatuma reminders.

Wewe unabaki bosi

Unaona chat zote kwenye inbox moja, unachukua mazungumzo wakati wowote, na unapata taarifa WhatsApp pale agent anapokuhitaji.

Vilivyomo

Bei zilizothibitishwa

Kila bei kwenye jibu inahakikiwa na katalogi yako kabla ya kutumwa.

Order & Booking

Order, delivery, pickup na appointment zinaingia kwenye calendar yako na reminders kwa mteja na kwako.

Wateja wanahifadhiwa wenyewe

Kila mteja anahifadhiwa na jina na eneo lake, tayari kwa follow-up na campaigns.

Campaigns na bulk messages

Templates zilizoidhinishwa na Meta, opt-out na mipaka ya mara ngapi unamtumia mteja.

Handover kwa mmiliki

Refund, malalamiko na mteja anayetaka mtu halisi vinakuja kwako na muhtasari.

Ripoti

Mazungumzo, leads, order na mapato kwa siku na kwa mwezi.

Kwa biashara zinazouza kupitia WhatsApp

Duka la mabati na vifaa vya ujenzi, simu na electronics, pharmacy, saluni, boutique, mgahawa, hoteli, shule: kama wateja wanakuandikia, Moran anakufanyia kazi.

Mabati na vifaa vya ujenziSimu na electronicsPharmacySaluniBoutiqueMigahawaHoteli na utaliiShuleNyumba na viwanjaSpare parts

Soma zaidi

Maswali ya mara kwa mara

Ndiyo. Moran inaunganisha kupitia WhatsApp Business Platform ya Meta kwa Embedded Signup rasmi. Namba inabaki yako, na sheria za Meta za templates na opt-out zinafuatwa moja kwa moja.

Siku 5 za kwanza ni bure bila kadi. Baada ya hapo unalipa mpango wa mwezi kwa Moran, na Meta inatoza kando kwa kila ujumbe unaoanzishwa na biashara (marketing, utility, authentication). Kumjibu mteja aliyekuandikia ndani ya saa 24 ni bure upande wa Meta.

Ndiyo. Anatambua lugha ya mteja na anajibu kwa Kiswahili cha kawaida cha Tanzania, Kiingereza, au mchanganyiko.

Hapana. Bei, stock na maelezo ya bidhaa vinatoka kwenye katalogi yako tu, na kila jibu linahakikiwa kabla ya kutumwa. Kama kitu hakipo kwenye data yako, anasema atathibitisha.

Agent anakukabidhi mazungumzo, anamwambia mteja mhusika atamjibu, na anakutumia muhtasari WhatsApp na email. Unajibu kutoka dashboard au simu yako.

Hapana. Unaunganisha namba ya WhatsApp Business unayotumia sasa.

Weka WhatsApp yako kwenye
autopilot leo.

Bure siku 5. Bila kadi. Unaweza kusitisha wakati wowote.

Anza bure siku 5