AI Agent ยท Tanzania

AI agent anayefanya kazi kwa biashara yako saa 24

Si chatbot ya vitufe. Moran ni AI agent anayeelewa maana ya ujumbe wa mteja, anatumia bei na stock halisi, anaweka order, anapanga appointment na anajua wakati wa kukuita.

Anza bure Omba demo

Chatbot na AI agent: tofauti ni nini?

Chatbot inafuata script na inakwama mteja akiandika kitu kisichotarajiwa. AI agent anasoma ujumbe, anakumbuka mazungumzo, anaangalia data ya biashara yako, anachukua hatua kama kuweka order au booking, na anajieleza kwa lugha ya mteja. Moran amejengwa kwa jinsi Watanzania wanavyochati: ujumbe mfupi, Kiswahili na Kiingereza vikichanganywa, picha, voice notes.

Anaelewa muktadha

"50?" baada ya kuuliza mabati ina maana bati hamsini. "kmy" ina maana mteja anasubiri. Agent anafuata mazungumzo badala ya kuuliza tena.

Anachukua hatua

Anaweka order, anapanga delivery na pickup, anahifadhi wateja, anatuma reminders, anatuma picha, anaangalia order.

Anajua mipaka yake

Refund, migogoro, malalamiko na mazungumzo ya bei nje ya sheria zako yanakuja kwako moja kwa moja na muhtasari.

Siku ya kawaida ya agent

Asubuhi

Anajibu ujumbe wa usiku, anathibitisha order za jana, na anakutumia ratiba ya booking na delivery za leo.

Mchana

Anatoa bei, anatuma picha, anahesabu jumla, anachukua order mpya, anapanga appointment na anakumbusha mteja saa moja kabla.

Anapokuhitaji

Anakuletea kesi ngumu na muhtasari wa nani, nini na kiasi gani, ili ujibu kwa dakika moja.

Jioni

Anafuatilia leads zilizonyamaza, anasasisha wateja na majina na maeneo, na anakuachia ripoti.

Kinachomfanya Moran awe tofauti

Injini tatu za AI zinazochaguliwa kwa kazi

Majibu ya kawaida, maombi magumu ya hatua nyingi na kesi nyeti kila moja inaenda kwa model inayoifaa. Majibu ya haraka, gharama ndogo.

Ukweli kwanza

Kila jibu linahakikiwa na katalogi na knowledge base. Hakuna bei za kutunga, picha za uongo au order zisizowekwa.

Kumbukumbu kwa kila mteja

Jina, eneo, bajeti, bidhaa anayopenda na order za nyuma vinakumbukwa, kwa biashara yako tu.

Anamtambua mmiliki

Unamwagiza agent kutoka WhatsApp yako kwa nenosiri la siri: bei mpya, sera mpya, bidhaa mpya.

Wafanyakazi wenza na ruhusa

Wape wafanyakazi inbox, bidhaa au campaigns bila kuwapa billing au settings.

Sauti na mitandao

Agent huyo huyo anajibu voice notes kwa sauti na anakusaidia kuendesha kurasa zako za kijamii.

Nani anatumia AI agent Tanzania

Maduka, wasambazaji, kliniki, shule, watalii na biashara za huduma zinazopata ujumbe mwingi kuliko mtu mmoja anavyoweza kujibu vizuri.

Rejareja na jumlaWasambazajiKliniki na pharmacyUtalii na safariElimuUkarabati na hudumaKilimo biasharaUsafirishaji

Soma zaidi

Maswali kuhusu AI agent

Agent anaongea kama mfanyakazi wako na anatumia jina unalompa. Hajifanyi binadamu mteja akiuliza moja kwa moja, na unaweza kuchukua mazungumzo wakati wowote.

Ndiyo. Weka nyaraka na maelekezo kwenye knowledge base, au mwandikie agent wako kutoka namba ya mmiliki na nenosiri: anahifadhi maelekezo na anayafuata.

Ndiyo. Huduma zenye bei, appointment na booking zinapangwa kwenye calendar yako na pande zote zinakumbushwa.

Anasema hivyo na anaahidi kuthibitisha, au anakukabidhi mazungumzo. Hatunguzi bei, stock, sera au gharama za delivery.

Kiswahili na Kiingereza, pamoja na mchanganyiko, na anafuata mtindo wa mteja.

Hapana. Data yako inatumika kuhudumia biashara yako tu.

Ajiri AI agent asiyepumzika.

Bure siku 5. Setup ndani ya saa moja.

Anza bure