Automation ya WhatsApp ยท Tanzania

Automation ya WhatsApp kwa biashara za Tanzania

Moran anaigeuza namba yako ya WhatsApp Business kuwa mfanyakazi asiyechoka: anajibu kila mteja ndani ya sekunde, kwa Kiswahili au Kiingereza, anatoa bei halisi kutoka katalogi yako, anaweka order na booking, na anakukabidhi pale mtu halisi anapohitajika.

Anza bure Ongea nasi

Automation ya WhatsApp ina maana gani kwa biashara ya Tanzania

Wateja wengi Tanzania wananunua kupitia WhatsApp. Wanauliza "bei?", "ipo?", "mnaleta Mbezi?" saa nne usiku na wanataka jibu sasa. Automation ina maana maswali hayo yanajibiwa mara moja na kwa usahihi bila wewe kushika simu siku nzima, na chochote kinachohitaji wewe, refund, mazungumzo ya bei, mteja aliyekasirika, kinakuja kwako na muhtasari.

Anajibu ndani ya sekunde

Bei, stock, eneo la delivery, saa za kazi, picha: majibu ya papo hapo kutoka data yako.

Anaandika kama wateja wako

Kiswahili, Kiingereza au mchanganyiko, hata "bei?", "kmy", "upo?".

Anauza

Anahesabu jumla, anaweka order, anapanga delivery au pickup kwenye calendar yako, na anafuatilia mwenyewe.

Hatua nne

Unganisha namba

Kupitia Meta Embedded Signup rasmi. Hakuna coding, hakuna simu za watu wengine.

Weka katalogi na maelezo

Bidhaa, bei, stock, picha, gharama za delivery, sera.

Mwache agent ajibu

Anajibu, anaweka order na booking, anahifadhi wateja, anatuma reminders.

Wewe unaangalia

Inbox moja, unachukua mazungumzo kwa mbofyo mmoja, unapata taarifa WhatsApp anapokuhitaji.

Vilivyomo kwenye automation ya Moran

Bei na stock zilizothibitishwa

Kila bei inahakikiwa na katalogi kabla ya kutumwa.

Order na booking

Zinaingia kwenye Order & Booking calendar na reminders kwa pande zote.

Wateja wanajihifadhi

Jina na eneo la kila mteja vinahifadhiwa kwa follow-up na campaigns.

Campaigns na bulk

Templates za Meta, opt-out na mipaka ya mara ngapi.

Handover kwa mmiliki

Refund, malalamiko na maombi ya mtu halisi yanakuja kwako na muhtasari.

Ripoti

Mazungumzo, leads, order na mapato.

Kwa biashara zinazouza WhatsApp

Duka la mabati linalotoa bei ya bati 50, muuzaji wa simu anayetuma picha, pharmacy inayothibitisha stock, saluni inayochukua booking.

Mabati na vifaa vya ujenziSimu na electronicsPharmacySaluni na spaBoutiqueMigahawaHoteli na utaliiShuleNyumbaSpare parts

Soma zaidi

Maswali kuhusu automation ya WhatsApp

Ndiyo, kupitia WhatsApp Business Platform ya Meta na Embedded Signup rasmi. Namba inabaki yako.

Siku 5 bure bila kadi. Baada ya hapo mpango wa mwezi kwa Moran; Meta inatoza kando kwa ujumbe unaoanzishwa na biashara. Kumjibu mteja aliyekuandikia ndani ya saa 24 ni bure upande wa Meta.

Ndiyo, Kiswahili cha kawaida cha Tanzania, Kiingereza au mchanganyiko.

Hapana. Bei zinatoka kwenye katalogi yako tu na kila jibu linahakikiwa kabla ya kutumwa.

Agent anakukabidhi, anamwambia mteja mhusika atamjibu, na anakutumia muhtasari.

Hapana, unatumia namba yako ya sasa ya WhatsApp Business.

Biashara nyingi zinaunganisha namba na kuweka bidhaa za kwanza ndani ya saa moja.

Weka WhatsApp yako kwenye
autopilot leo.

Bure siku 5. Bila kadi.

Anza bure